BLINKEN AZURU BARA LA AFRIKA KUFUKIA MASHIMO YA TRUMP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken yuko nchini Afrika Kusini kuanza ziara yake ya pili barani Afrika kugeuza ukurasa wa Trump na kukabiliana na ushawishi wa Urusi na China.

Wakati midahalo ya mara kwa mara huko nyuma,ilikoma kufanyika chini ya utawala wa Donald Trump ambaye alionyesha nia ndogo katika mahusiano na Afrika na sasa utawala wa Biden unataka kuanza vizuri na washirika wake katika bara la Afrika.

Mataifa hayo mawili hayaafikiani katika ngazi ya kidiplomasia kwa vita vya Ukraine,Afrika Kusini ambalo ni sehemu ya BRICS imeendelea kupinga kulaani Urusi,huku ikipendelea kuwa na msimamo usioegemea upande wowote.

Nchi hizi mbili zitajadili kuhusu masuala ya kiuchumi,wakati Marekani ni mshirika wa tatu wa kibiashara wa Afrika Kusini baada ya Uchina na Ujerumani na moja ya vyanzo vikuu vya watalii wa kimataifa kwa nchi hiyo.

Antony Blinken atapaswa kuwasilisha mkakati mpya wa Marekani kwa Afrika,ambao unalenga kuimarisha ushawishi wa Washington katika kukabiliana na nchi zenye nguvu zinazokinzana,bila kufanya nchi za Afrika kuwa chambo kwenye masuala ya kisiasa.

Post a Comment

0 Comments