MAKATIBU MUHTASI WA MAHAKAMA WAPEWA MAFUNZO

Makatibu Muhtasi wanaoshiriki katika mafunzo  ikifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mkuu wa Chuo.

*************
Na.Rosena Suka,Lushoto

Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo,  Jaji wa Mahakama ya Rufaa na Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto,tarehe 9 Agosti, 2022 amefungua mafunzo ya siku tano kwa Makatibu Muhtasi 56 wa Mahakama ya Tanzania  yanayohusu  Namna Bora ya Uendeshaji wa Ofisi. 

Akifungua mafunzo hayo Mhe. Dkt. Paul F. Kihwelo amewataka Makatibu Muhtasi  kutoa huduma bora zinazoendana na uwekezaji katika majengo ya Mahakama nchini.  

Mahakama ya Tanzania iko katika maboresho ambayo yanagusa maeneo mbalimbali ikiwemo miundombinu ya majengo na raslimali watu hivyo mafunzo haya,yanalengo la kuwaandaa watumishi hao kuendana na mabadiliko yanayoendelea.

“Lengo la mafunzo yanayotolewa ni kujaribu kuwajengea uwezo na kubadilishafikra za watumishi wa Mahakama ili huduma wanazozitoa mahakamani ziendane naubora wa majengo ambayo yanaendelea kuboreshwa,” amesema.

Mhe.Dkt.Kihwelo aliwasihi watumishi hao kuwa waadilifu na wachapakazi ili kuipasifa  nzuri  Mahakama ya Tanzania kwa kuepuka vitendo vinavyoweza kuichafuaMahakama kama matumizi ya lugha mbaya. Pia aliwaomba watumishi haowatakaporudi kwenye vituo vyao vya kazi ni wajibu  kushirikiana na kuonyeshawaliochojifunza.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama yaTanzania, Bi. Beatrice Patrick amewaambia washiriki hao kuwa Mahakamaimejipanga kuwajengea uwezo watumishi wake katika kada mbalimbali ili kuendanana maboresho yanayoendelea.

Bi.Beatrice Patrick amesema kundi hilo la washiriki wa mafunzo linajumuishaMakatibu Muhtasi 56, ambapo 50 wametoka katika Mahakama mbalimbali zaMwanzo, Mahakama za Wilaya na Mahakama za Hakimu Mkazi,  washiriki  sitawakiwa ni waajiriwa wapya.

Amesema watumishi hao wanapewa mafunzo kwa lengo la kuwakumbusha majukumu yao ya kazi za Ukatibu Muhtasi,utunzaji wa kumbukumbu,usimamizi wa ofisi na mawasiliano ya kiofisi,uzalendo na protokali,mipango ya Mahakama na uboreshaji,huduma kwa mteja, masuala ya saikolojia na ushauri.

Mwelekeo wa Mahakama kwa sasa katika mapinduzi ya viwanda kuelekea Mahakama Mtandao na matumizi ya TEHAMA.

Post a Comment

0 Comments