MIAKA 20 JELA KWA KUSAFIRISHA MIKOKO

Shehena ya Mikoko iliyokamatwa katika Bandari bubu ya Bagamoyo

Muhifadhi Msaidizi Daraja la Pili Issa Mziray akionyesha shehena ya mikoko iliyokua inasarishwa kupitia bandari bubu.

Muhifadhi Msaidizi Daraja la Pili Issa akizungumza na waandishi wa Habari

*************
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS)limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano ili kuweza kuwabaini watu wanaoenda kinyume na utaratibu katika utunzaji wa rasilimali za misitu.

Mahakama imemhukumu mtu huyo kwenda jela miaka ishirini (20)aliyekamatwa akisafirisha miti aina ya mikoko ambazo ni rasilimali za misitu kupitia bandari bubu

Hayo yamebainishwa na Meneja wa TFS wilaya ya Tanga,Muhifadhi Msaidizi Daraja la Pili Issa Mziray,ameeleza kuwa walikamata miti ya mikoko iliyokuwa inasafirishwa katika bandari bubu ya bagamoyo na mtuhumiwa kupelekwa mahakamani.

"Mwaka jana zilikamatwa miti ya mikoko katika bandari bubu ya Bagamoyo,kesi ilikwenda mahakamani kitengo cha uhujumu uchumi Mahakama Kuu na mtuhumiwa alitiwa hatiani na kufungwa kifungo cha miaka 20 na mali zake zote kutaifishwa"alisema Mziray

Aidha Mziray amesema kuwa katika operesheni nyingine walizopata wamefanikiwa kukamata jumla magunia 190 ya mkaa,katika bandari bubu ya mapuani,wamefanikiwa kukamata trekta katika bandari ya bubu ya Stahabu ikiwa imebeba magogo ambapo mali zake zilitaifishwa.

"Wengi wawanaopatikana na makosa hukiri makosa yao na hivyo kulipa faini"alisema Mziray.

Ameeleza kuwa baadhi ya maeneo yenye sifa mbaya zinazotumiwa na watu wasio waaminifu kusafirisha maliasili zao haramu kutoka wilayani humo hadi nje ya nchi ni pamoja na Makuani,Kichalikani,Bombani na Boma,zote za wilayani Mkinga,maeneo ya wilaya ya Tanga,ni Chongeleani na Bagamoyo.

Alisema Pangani ina vijiji vinne ambavyo vinajihusisha na biashara ya magendo ambazo ni Makuani,Kipumbwi Mtoni,Sange,Stahabu na Buyuni.

Mziray amesema mafanikio ya operesheni hizo,wanakijiji wana mchango mkubwa katika kuwakamata wahalifu hao. 

Post a Comment

0 Comments