NATIONAL NCDs RESEARCH AGENDA YAZINDULIWA..WATAFITI WATAKIWA KUJA NA MAJIBU SHAHIDI

Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt.Aifello Sichwale akikata kuashiria uzinduzi wa Agenda ya utafiti ya magonjwa yasiyoambukiza NCDs,wanaoshuhudia ni Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Muhas Profesa Bruno Singuya,Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya,Dkt.Omary Ubuguyu.
Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt.Aifello Sichwale akizungumza kwenye uzinduzi wa Agenda ya Utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza NCDs .
Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Muhas Profesa Bruno Sunguya,akizungumza kwenye uzinduzi wa Agenda ya Utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza NCDs.
Katibu wa Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Prof.Kaushik Rumaiya,akizungumza kwenye uzinduzi wa Agenda ya Utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza NCDs.
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya,Dkt.Omary Ubuguyu,akizungumza kwenye uzinduzi wa Agenda ya Utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza NCDs.
Afisa Uhusiano Mwandamizi MUHAS Helen Mtui akifanya utambulisho kwenye,
kwenye uzinduzi wa Agenda ya Utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza NCDs.
Washiriki wa Taasisi mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa Agenda ya Utafiti wa magonjwa yasiyoambukiza NCDs.

*************
National NCD's Research Agenda ambao umeratibiwa na Wizara ya Afya,Chuo Kikuu cha Sayansi Shirikishi(MUHAS)pamoja na Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Tanzania(Tanzania Diabates Association TDA)umezinduliwa na Mganga Mkuu wa Serikali,agenda inalenga kupunguza vifo kabla ya umri usiotarajiwa kwa kuwekeza katika utafiti wa kinga ili kukabiliana na madhara ya magonjwa yasiyoambukiza.

Mganga Mkuu wa Serikali,Dkt.Aifello Sichwale amewataka wataalamu kutoka vyuoni wajikite zaidi katika utafiti ili kuweza kuja na majibu sahihi,yatakayoweza kuleta usuluhishi katika magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza.

Takwimu zinaonyesha kuwa magonjwa ambayo sio ya kuambukiza yanaongezeka kwa asilimia 17 kwa dunia nzima,huku katika bara la Afrika ongezeko likiwa ni kwa asilimia 24.

Dkt.Sichalwe amesema kupitia NCDs Reserch Agenda ni vema wakatumika wanafunzi wa Vyuo Vikuu walio katika ngazi za Shahada ya kwanza na Shahada ya Uzamivu ili waje na majibu shahidi katika eneo la magonjwa yasiyoambukiza.

"Kupitia mpango huu tunataka kuongeza tafiti shahidi,katika eneo hili uzoefu unaonyesha katika sekta hii kumekua na wadau wachache sana ambao wanafanya tafiti,jambo linalofanya takwimu zisipatikane kwa usahihi,kwa namna inavyotakiwa"alisema Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Sichwale

"Shirika la Afya Duniani lilikadiria kwamba kwa muongo ambao tupo,magonjwa yasiyo ya ambukiza yangeongezeka kwa asilimia 17 Duniani,na katika Afrika yangeongezeka kwa Asilimia 24,hasara kubwa imekua ikitokea kwa mtu mmojammoja,lakini familia na Serikali ndio zimekua zikiathirika,kwa kuwa familia ikiwa na mgonjwa uwajibikaji wa mgonjwa umekua wakusuasua katika uzalishaji katika familia,jambo linaloleta hasara kwa Serikali"alisema Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Sichwale.

Hata hivyo Dkt.Sichwale amesema magonjwa yasiyoambukiza nchini Tanzania,takwimu za mwaka 2018 zinaonyesha kuwa magonjwa yasiyoambukiza yamekua yakichangia vifo kwa asilimia 33 kwa magonjwa yote.

"Tukiunganisha nguvu ya pamoja kwa watu ambao wameathirika madhara yanaweza kupungua kwa vizazi vijavyo,kwa kutoa elimu kuhusu namna bora ya kuishi na kuacha tabia bwete ya kukaa sehemu moja kwa muda mrefu,sambamba na kuzingatia utaratibu wa kula vyakula kwa mpangilio"alisema Mganga Mkuu wa Serikali Dkt.Sichwale

Naye Mwakilishi wa Mkuu wa Chuo cha Muhas Profesa Bruno Sunguya,amesema kuwa kwa sasa Chuo Kikuu cha Muhimbili imeanza kuweka jitihada za utafiti katika ufundishaji,kwa kuweka kipaumbele za utafiti katika magonjwa yasiyoambukiza ili kuboresha maisha ya watu.

"Kutokana na Mabadiliko mbalimbali ya mifumo ya maisha,maendeleo ya kijamii pamoja na maendeleo ya kiuchumi,magonjwa yasiyoambukiza yamekua yakiongezeka,ongezeko lake yamekua yakileta mabadiliko katika jamii,jambo lililofanya Chuo cha Muhimbili kuboresha mbinu za ufundishaji na tafiti ili kuboresha maisha ya watu kuendana na magonjwa yasiyoambukiza"alisema Prof.Singuya

Naye Katibu wa Chama cha Ugonjwa wa Kisukari Prof.Kaushik Rumaiya,amesema kuwa agenda hiyo walivyouandaa,utaenda kugusa Hosptali za mikoa 27 na Hosptali za Wilaya 134 na Vituo vya Afya 484.

"Sisi kama nchi ili kukabiliana na magonjwa yasiyoambukiza nilazima kutoa kinga,kwa kuwa matibabu ya magonjwa haya ni garama sana,tunataka jamii isipate magonjwa haya na lengo kuu nikutoa kinga ili jamii isiweze kuathirika zaidi"alisema Dkt.Kaushik

Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba kutoka Wizara ya Afya,Dkt.Omary Ubuguyu amesema jambo kuu la kuzingatia zaidi ni kufanya magonjwa yasiyoambukiza yasilete madhara ya vifo katika umri usiotarajiwa.

"Kwenye NCDs mapambano yetu sio kwamba watu wasife kwa NCDs,mapambano yetu ni watu wasife kabla ya umri tarajiwa,huo ndio mpambano mkubwa tulionao"alisema Dkt.Ubuguyu.

Post a Comment

0 Comments