SITAKI KUJIHUSISHA NA MGOGORO WA MAREKANI NA RUSSIA

Rais wa Uganda Yoweri Museveni amesema kwamba nchi yake haitaagiza mafuta kutoka Russia kama alivyoomba waziri wa mambo ya nje wa Russia, Sergey Lavrov wakati wa ziara yake ya hivi karibuni nchini Uganda.

Museveni akizungumza na taifa,amesema kwamba licha ya Russia kutaka kuiuzia Uganda mafuta kwa bei rahisi lakini hataki kujiingiza katika mgogoro kati ya Marekani na Russia.

Serikali itatafuta mbinu mbadala za kuhakikisha kwamba kuna mafuta ya kutosha nchini Uganda, wakati inajitayarisha kutekeleza mikakati ya muda mrefu ikiwa ni pamoja na kuwa na nishati safi, magari na pikipiki zinazotumia nguvu za umeme.”

“Endapo tutanunua mafuta kwa bei rahisi kutoka Russia,ina maana kwamba tunakiuka vikwazo vya nchi za magharibi dhidi ya Russia,tangu tatizo lilipoanza,nimekuwa nikiwasiliana na viongozi wa Russia na Marekani,sasa mnaweza kuona mazungumzo yetu yameanza kuruhusu nafaka na ngano kusafirishwa kutoka Ukraine”alisema Museveni

“Sitaki kujiingiza katika mgogoro usionihusu moja kwa moja,njia ya kusuluhsisha uhaba wa bidhaa muhimu unaoshuhudiwa duniani kwa sasa ni kutumia diplomasia.

“Kama nataka kununua mafuta,ningeiambia Russia kusafirisha mafuta hayo hadi hapa na wangefanya hivyo,lakini hatua hiyo inatuweka katika matatizo na Marekani ambayo sio jambo zuri,kwa sasa tutumie vizuri mafuta tuliyo nayo huku tukitafuta mbinu mbadala”

Hotuba ya Museveni kwa taifa imejiri siku chache baada ya kukutana na mabalozi wa ngazi ya juu wa Russia na Marekani.

Post a Comment

0 Comments