Takriban wanajeshi watano wameuawa na wengine kujeruhiwa katika mlipuko wa barabarani uliolenga vikosi vya Umoja wa Afrika nchini Somalia siku ya Jumamosi.
Msafara wa Kikosi cha Mpito cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (ATMIS) ulikanyaga bomu la kutegwa ardhini kwenye mitaa ya Marka, mji mkuu wa mkoa wa kusini magharibi mwa eneo la Lower Shabelle.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya ndani,Wanajeshi watano waliouawa walikuwa ni wa Uganda na walikuwa wakihudumu katika kikosi hicho cha Umoja wa Afrika,Kundi la kigaidi la al-Shabaab limedai kuhusika na shambulio hilo.
Umoja wa Mataifa umekuwa ukifadhili askari wa Umoja wa Afrika wapatao 21,000,ambao wamekuwepo nchini Somalia tokea mwaka 2007.
Wanajeshi wa AMISOM ni kutoka Uganda,Kenya,Burundi,Somalia, Ethiopia,Djibouti na Sierra Leone,huku maafisa wa polisi wa kikosi hicho cha AU wakitoka Nigeria, Sierra Leone na Uganda.

0 Comments