USAJILI KWA WAHAMIAJI WASIO RASMI WAANZA

Wakazi wa kjiji cha Duga Maforoni wakiwa katika foleni ya kusajiliwa.

Dkt.Kassim Sufi  Mwakilishi wa Shirika la Wahamiaji Duniani (IOM)

Shirika la wahamiaji Duniani (IOM)imeanza zoezi la msaada wa usajili kwa Wahamiaji wasio rasmi ambao unashughulikia mikoa 11 hapa nchini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi ilo Mwakilishi wa Shirika la Wahamiaji Duniani Dkt.Kassim Sufi amesema zaidi ya wahamiaji 30000 wanaishi katika mkoa wa Tanga.

Usajili umezinduliwa katika wilaya ya mkinga ambapo kauli mbiu yake ni JIANDIKISHE UTAMBULIKE.

"Leo tunaweza kusema kwamba tunaingia rasmi katika hatua muhimu ya kuhamasisha ufahamu wa zoezi.la usajili wahamaji wasio rasmi Tanzania ambayo itakua kwenye mikoa ya mipaka"

Katika mikoa hiyo 11 idara ya huduma ya uhamiaji Tanzania ikiungwa mkono na IOM itafanya usajili kwa wahamiaji wote wasio rasmi.

Hata hivyo Dkt.Kassim amesema kupitia usajili huo Serikali ya Tanzania itatoa uamuzi wa utambulisho na kutoa huduma za msingi,kijamii kwa wahamiaji wanaostahiki.

Dkt.Kassim amesema jamii Watanzania wengi wamekua wakarimu kwa kuwakaribisha watu kutoka nchi jirani na Tanzania imebaki kuwa salama kwa wale wanaokimbia njaa,na mizozo katika nchi jirani na kuwakaribisha watu wenye mahitaji tangu enzi za Baba wa Taifa.


Naibu Katibu mkuu Wizara ya Mambo ya ndani Ramadhan Kailima akizungumza na katibu tawala wilaya ya mkinga Joseph Sura,kulia ni 
Dkt.Kassim Sufi  Mwakilishi wa Shirika la Wahamiaji Duniani (IOM) na Afisa kutoka (IOM) Halima Kassim.

Post a Comment

0 Comments