Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation,Doris Mollel akikabidhi msaada wa futari kwa mkazi wa Mabokweni,Tanga walipokwenda kutoa futari kwa kaya zenye changamoto ya Futari ya kila siku katika mwezi huu wa Toba.
Mratibu msaidizi wa TIKA Badru Yasin aliyevaa kaushi akiwa na wakazi wa Mabokweni walipokwenda kutoa Futari kwa kaya zenye changamoto ya Futari ya kila siku.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Doris Mollel Foundation Doris Mollel akikabidhi Futari kwa mnufaika wa Futari katika mwezi huu Toba.
Mratibu msaidizi wa TIKA Badru Yasin akizungumza na baada ya kutoa futari kwa kaya zenye changamoto ya Futari ya kila siku.
Waziri wa TAMISEMI na Mbunge wa Tanga Ummy Mwalimu akiwa na Doris Mollel kutoka Doris Foundation na mratibu msaidizi wa TIKA Badru Yasin walipokuwa wakigawa Futari kwa kaya zenye changamoto ya Futari ya kila siku.
********************
Taasisi ya TIKA kutoka Nchini Uturuki inayoratibu shughuli za Maendeleo ya Jamii hapa nchini imetoa msaada kwa kaya 200 zenye changamoto ya kupata futari ya kila siku mkoani Tanga.
Kaya zilizopatiwa msaada huo ni wa kata ya Mzizima na Mabokweni ambazo zipo nje kidogo ya jiji la Tanga.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi vyakuka hivyo Mratibu msaidizi wa TIKA Badru Yasin amesema wameamua kutoa Futari kwa kaya maskini ili waweze kufunga vizuri katika mwezi huu wa Toba.
Amesema kuwa msaada huo hauishi katika jiji la Tanga tu bali wataenda kwenye baadhi ya miji hapa nchini na wanatarajia kufikia kaya 3000 kwa Tanzania bara na Zanzibar.
Kwa mwaka huu wameshirikiana na Doris Mollel Foundation katika kuhakisha kaya maskini zinapata futari bila kuwa na changamoto zingine zitakazowasumbua katika funga yao.
Katika zoezi hilo Mbunge wa Jimbo la Tanga na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Ummy Mwalimu alikuepo katika zoezi hilo la wananchi wake wenye changamoto ya Futari ya kila siku walipogawiwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani kukumbukwa.
"Tunawashukuru sana kwa kuwakumbuka kaya 200 na kuwapongeza Doris Mollel Foundation na TIKA,ziko kaya ambazo zinashindwa kumudu futari katika kipindi hiki cha mfungo,tumepokea mahitaji ni makubwa,natamani wadau wengi zaidi wangejitokeza,wakatuunga mkono kwa futari kwa kaya,watu wanafunga na inapendeza jioni mtu akifutari apate nguvu ya kuendelea kufunga"
0 Comments