ETHIOPIA WAREJESHA DIPLOMASIA NA SOMALIA


Ethiopia na Somalia wamerejesha uhusiano kamili wa kidiplomasia Nchi hizo mbili pia zilisema zimejitolea kuheshimu makubaliano ya hivi majuzi waliyotia saini mjini Ankara kufuatia mazungumzo ya upatanishi wa Uturuki.

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud aliwasili Ethiopia Jumamosi kwa ziara yake ya kwanza rasmi tangu mazungumzo ya upatanishi ya Uturuki kutatua mizozo ya muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili.

Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed alimkaribisha Mohamud kwa mapokezi ya hali ya juu,na viongozi hao wawili walifanya majadiliano yaliyojikita katika kuimarisha uhusiano na kushughulikia vipaumbele vya pande zote, kulingana na chapisho la Ahmed kwenye X.

Mazungumzo kati ya viongozi hao wawili yalizingatia haja ya kuendelea na kuimarisha ushirikiano wa kiusalama wa nchi hizo mbili,kwa mujibu wa taarifa ya pamoja iliyotolewa mwishoni mwa majadiliano yao.

''Walikubali kurejesha na kuimarisha uhusiano wa nchi mbili kupitia uwakilishi kamili wa kidiplomasia katika miji mikuu yao,'' iliongeza taarifa hiyo.

Post a Comment

0 Comments