ASKARI WA ISRAEL AIBUKIA BRAZIL

Mwanajeshi wa Israel anayetuhumiwa kufanya uhalifu wa kivita wakati wa vita vya Gaza amekimbia Brazil ambapo mamlaka zilikuwa zikishinikiza uchunguzi ufanyike, vyombo vya habari vya ndani vimesema.

Uchunguzi huo unatokana na malalamiko yaliyowasilishwa na Hind Rajab Foundation (HRF), shirika lenye makao yake Ubelgiji linalotetea haki kwa wahanga wa Palestina, shirika la utangazaji la Israel KAN lilisema.

Kulingana na Idhaa ya 12 ya Israel, malalamiko hayo yanajumuisha zaidi ya kurasa 500 za ushahidi, zikiwemo video, data ya eneo la kijiografia, na taarifa za kijasusi za chanzo huria, zinazohusisha askari huyo na uharibifu huko Gaza.

HRF ilitaka askari huyo azuiliwe mara moja ili kuzuia kutoroka kwake au uharibifu wa ushahidi, kituo hicho kilisema.

Post a Comment

0 Comments