BILIONEA MULOKOZI AKABIDHI ZAWADI YA BAJAJI MPYA KWA KIJANA ALIYEWEKA PICHA YAKE

Bilionea David Mulokozi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati Super Brands Limited ametoa zawadi ya Bajaji mpya kwa Dereva wa bajaji Abel Rajabu ambaye ameweka picha ya Bilionea huyo kwenye bajaji yake baada ya kuvutiwa na kazi anazozifanya za kuwekeza kwenye viwanda na kusaidia jamii inayomzunguka kutokana na faida anayoipata.

David Mulokozi amempongeza kijana huyo kwa kuweka picha yake kwenye bajaji kutokana na upendo wa dhati alionao ambapo aliamua kuweka picha hiyo kwenye bajaji kama zawadi kwake suala lilomgusa Mkurugenzi huyo na kuamua kutoa zawadi ya bajaji.

“Bajaji hiii itamsaidia kuongeza kipato chake ,Namshukuru sana alifanya hivyo kwa mapenzi ya dhati kwangu kwani nimetoa hamasa kwa vijana wengi wa kitanzania kufanya kazi kwa bidi na kutimiza ndoto zao huku wakiendelea kusaidia jamii inayowazunguka” Anaeleza Mulokozi

Mkurugenzi huyo wa Mati ametoa wito kwa madereva wa bajaji kutangaza bidhaa zinazozalishwa na kiwanda chake ikiwemo Tanzanite Royal Gin,Strong Dry Gin na Tanzanite Premium Vodka .

Kwa upande wake Dereva huyo wa Bajaji Abel Rajabu ameeleza kufurahishwa na zawadi hiyo ya bajaji mpya kwani hakutegemea aliweka picha ya Biionea huyo baada ya kuvutiwa na kazi anazozifanya zilizotangazwa katika vyombo vya Habari na mitandao ya kijamii.

Abel amemshukuru Mulokozi kwa moyo wa upendo na kujitolea kusaidia jamii inayomzunguka Pamoja na kutoa fursa za ajira kwa vijana wengi kupitia viwanda vyake.

Post a Comment

0 Comments