BALAMA MAPINDUZI KWENDA AFRIKA KUSINI.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya Yanga SC Mapinduzi Balama muda wowote kuanzia sasa atapelekwa nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

Balama alipata maumivu ya mguu wa kushoto msimu uliopita wakati timu yake ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ndanda FC.

Kwa sasa ameendelea kupewa huduma ya matibabu huku akishuhudia wenzake wakiendelea kupambana kupata matokeo ndani ya uwanja.

Daktari wa Yanga, Shecky Mngazija amesema kuwa kiungo huyo atakwenda Afrika Kusini ili kufanyiwa uchunguzi zaidi baada ya kukosekana uwanjani kwa muda mrefu.

"Ni kweli Balama Mapinduzi anaelekea Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa zaidi vipimo vya afya yake ili kuendelea mchakato na maendeleo yake.


Post a Comment

0 Comments