Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali kuhusu Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA), unaofanyika Kigali nchini Rwanda tarehe 19 Mei, 2026.
Mkutano huo wa kimataifa umewakutanisha viongozi wa serikali, wataalamu wa nishati, wawekezaji pamoja na mashirika mbalimbali ya kimataifa kujadili matumizi ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Bara la Afrika.
Aidha, mkutano huo unalenga kujadili namna bora ya kuongeza upatikanaji wa nishati ya umeme Afrika, kupunguza uchafuzi wa mazingira, kusaidia maendeleo ya viwanda, kukuza ubunifu wa teknolojia za nishati ya nyuklia pamoja na kuvutia wawekezaji katika miradi ya nishati kwa maendeleo endelevu ya Afrika.







0 Comments