FIKA BRELA UPATE HUDUMA ZA HATAZA NA MILIKI BUNIFU

Afisa Msajili msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA),Bethod Bangahonoze akiwa ndani ya kliniki ya Biashara.

Afisa Msajili msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni(BRELA),Bethod Bangahonoze akiwa ndani ya kliniki ya Biashara.

***********

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni hapa nchini(BRELA)imewataka wananchi kufika katika mabanda yao,kupata huduma za hataza na miliki bunifu,kwenye Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayofanyika katika viwanja vya Sabasaba.

Akizungumza kwenye maonyesho hayo Afisa Msajili msaidizi wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni,Bethod Bangahonoze amesema kuwa wanatoa huduma za usajili wa makampuni na majina ya biashara.

"Kwa mwananchi yeyote ambae amepata changamoto kwenye namna ya kupata huduma za BRELA,afike katika banda kwa msaada zaidi,kwenye maonyesho hayo wanamabanda matatu,na sehemu zote maafisa wa BRELA wapo wakiendelea kutoa huduma.

Bethod ameongeza kuwa,BRELA kwa sasa wanaendelea kutoa huduma za hataza na miliki bunifu na wanatoa leseni za biashara daraja A,zenye sura ya kimataifa,pamoja na leseni za viwanda.

Post a Comment

0 Comments