Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, ameweka jiwe la msingi la Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi ya Bahari, Buyu,
Akizungumza baada ya kuweka jiwe la Msingi Januari 05, 2025 Zanzibar Dkt. Mwinyi amesema kuwa taasisi hiyo itasaidia kuendeleza uchumi wa bluu kupitia tafiti na mafunzo ya wataalamu wa sekta za uvuvi, utalii, na mazao ya baharini.
Ameongeza kuwa Mradi huo wa zaidi ya Shilingi bilioni 11 unaofadhiliwa na Benki ya Dunia utaboresha elimu ya juu na kuongeza wataalamu wa uchumi wa bluu.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda, amesema mkopo wa shilingi bilioni 972 kutoka Benki ya Dunia utaimarisha vyuo vikuu nchini kwa kuboresha miundombinu, kuongeza ufadhili kwa wahadhiri, na kuanzisha programu mpya.
Prof. Mkenda amempongeza Rais Mwinyi kwa juhudi kubwa katika kuimarisha sekta ya elimu, akisisitiza kuwa mageuzi hayo ni msingi wa maendeleo endelevu ya taifa.
0 Comments