Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema yuko tayari kuwarejesha nchini mwao wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini waliotekwa,kwa mabadilishano ya kuachiliwa huru wafungwa wa kivita raia wa Ukraine walioko Urusi.
Pendekezo la Zelensky amelitoa saa chache baada ya idara ya kitaifa ya ujasusi ya Korea Kusini kuthibitisha tangazo la siku iliyopita kwamba Ukraine imewakamata wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini.
Mamlaka nchini Ukraine siku ya Jumamosi ilisema wanajeshi hao wawili walijeruhiwa vibaya katika uwanja wa vita wakati wakipambana na wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Kursk nchini Urusi, lakini wakati huo hawakutoa ushahidi kuthibitisha uraia wao.
Hata hivyo, jana Jumapili, Idara ya ujasusi ya Korea Kusini NIS imeliambia shirika la habari la AFP kwamba, imethibitisha kuwa jeshi la Ukraine limewakamata wanajeshi wawili wa Korea Kaskazini mnamo Januari 9 katika uwanja wa vita eneo la Kursk, nchini Urusi.
0 Comments