M23 WASHAMBULIA MJI WA SAKE KWA MABOMU


Mapigano hayo karibu na mji wa Sake yalitokea siku ya Jumanne Januari 7 asubuhi kwenye mlima Kihuli na Kimoka kijiji kilichoko kilomita 5 kutoka  mji huo wa kimkakati.

Taarifa zinasema kuwa wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wanaosaidiwa na wanamgambo wazalendo, walizishambulia kwa mizinga ngome za waasi wa M23 waliojaribu kuushambulia mji wa sake kilomita 27 magharibi mwa mji wa Goma.

Wakati  mapigano yalikuwa yakiendelea,mabomu yalirushwa maeneo yanayokaliwa na waasi na kuangukia  katikati mwa mji wa Sake na kuwauwa watu wananne wakiwemo watoto na wanawake,kama anavyo eleza Batachoka Douglas raia aliyeshuhudia tukio hilo baya.

"Mapigano yalianzia huko Kihuli ambapo wazalendo walipambana na M23 ,majira ya sambili unusu waasi wa M23 wakatupa bomu katika mji wa Sake na kuwauwa watu watatu na mmoja kujeruhiwa ambaye alifariki pia saa chache akiwa hospitalini huko CEBCA Ndosho".

Upande mwingine katika wilaya hiyo ya Masisi, jeshi tiifu kwa serikali ya kongo, FARDC na vikundi vya wenyeji wenye silaha, vilichukua udhibiti wa vijiji vya Ruzirantaka, Kabingo, Kadahangwa na Kashovu kilomita nne kutoka mji mwingine unaokaliwa na M23 wa Ngungu, kama anavyobainisha raia huyu.

Post a Comment

0 Comments