Diwani wa kata ya Majengo Salim Perembo
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika kikao
Baadhi ya viongozi na wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakiwa katika kikao
*****************
Wanachama wa Chama cha mapinduzi wametakiwa wawe na uvumilivu na wasionyeshe chuki pindi demokrasia inapochukua nafasi yake wakati wa uchaguzi kwa upande mmoja unaoshindana ukishindwa.
Hayo yamebainishwa na Diwani wa kata ya Majengo Salim Perembo,wakati wa ziara ya Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa mkoa wa Tanga Mohamed Salim Ratco aliyoifanya katika wilaya ya Korogwe.
Perembo amesema uvumilivu unahitajika kwenye Chama kwa wakati wote,kabla ya uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Amesema kuwa uchaguzi ndio chanzo ya chuki ndani ya Chama kutokana na baadhi ya viongozi kuwa na makundi ambapo wakishindwa wanakosa kuwa na uvumilivu na matokeo yake kusababisha chuki baina ya wanachana kwa kuwa hawajafikia malengo yao waliyohitaji baada ya uchaguzi.
"Nataka niwasihi wanachama wa CCM tunakwenda kwenye uchaguzi uvumilivu subra,na msionyeshe chuki ya kuegemea upande mmoja haifai" alisema Perembo
Ameongeza kuwa inapofika wakati wa demokrasia fanya kinachostahili kwa kuona kipi kinakufaa na baada ya uchaguzi rudi kawaida na kuondokana na makundi ya uchaguzi.
"Unapokwenda kwenye uchaguzi fanya kinachostahili,uchaguzi ukiisha umeisha mnabaki wa moja na kuwa CCM wamoja,watakaokosa wawe wavumilivu na waliopata wafanye busara ya uongozi wao kuwaunganisha watu,kazi ya uongozi sikugawa watu ni kuwaunganisha watu" alisema Perembo
Pia amemwelezea MNEC mkoa wa Tanga Mohamed Salim kuwa ni mfano wa kuigwa kwani hakugawa watu na wala hakugawa wilaya na ndio maana anafanya ziara katika kila Wilaya.
0 Comments