Chama cha kulinda na kutetea haki za Walimu Tanzania ( CHAKUHAWATA) kimefanya mkutano mkuu Kitaifa na Kufanya uchaguzi wa viongozi mbalimbali wa chama hicho na kumchagua Bw. Emmanuel Patric Herman kuwa Mwenyekiti wa chama hicho
Mkutano huo wa CHAKUHAWATA umefanyika Jijini Tanga ambapo wajumbe walishiriki kuchagua viongozi hao kwa kuwapigia kura ya siri huku Bw Emanuel Herman ameshinda kiti cha uenyekiti kwa kupata kura 168 na mpizani wake ambae ndiye aliekuwa mwenyekiti aliepita Bw. Ashery Ntayomba amepata kura 106 huku jumla ya wapiga kura wote walikua ni 302
Pia chama hicho kimemchagua Rebeka Emmanuel kuwa Mwenyekiti Msaidizi na Bw. Twalb Nyamkunga ameshinda nafasi ya Katibu Mkuu pamoja na Elias Chanda yeye ameshinda nafasi ya Muwekahazina.
Chama hicho kilianza kikiwa na wanachama 180, na mpaka kufikia 2024 chama hicho kina wanachama zaidi ya 29000
0 Comments