MADEREVA WAJUE WANADHAMANA KUBWA SANA PINDI WANAPOKUWA BARABARANI

Mwenyekiti wa Usalama barabarani mkoa wa Tanga Rashid Liemba amewataka madereva wajue kuwa wanadhamana kubwa sana pindi wanapokua barabarani.

Liemba ameyasema hayo wakati wa utoaji elimu kwa madereva katika stand ya mabasi ya mkoa wa Tanga ilioyopo Kange,iliyoongozwa na Kamanda wa kikosi cha Usalama barabarani nchini Wilbroad Mutafungwa.

"Napenda kuwasihi madereva wajielewe kuwa wanadhamana kubwa sana,dhamana kubwa kupita kiasi,wakati unaendesha gari uelewe unaroho zaidi ya 60 ndani ya gari yako na zote zinakutegemea wewe,wakati tajiri kalala nyumbani kwake,kwa hivyo nachowasihi madereva,jitahidini kadri ya uwezo wenu kufanya muende taratibu" alisema Liemba.

Aidha ameongeza kuwa asilimia 90 ajali zinatokana na uzembe hivyo madereva wakizingatia sheria ajali haitakuwepo kabisa.

"Asilimia 90 za ajali Tanzania inatokana na uzembe,na kama uzembe hautakuwepo nina hakoka ajali itapungua kwa asilimia 90 vilevile hivyo ninawaomba madereva wajitahidi walinde magari yao na kulinda abiria waliowapakia." alisema Liemba.

Hata hivyo amesema katika mkoa wa Tanga kamati yake imejipanga  kuhakikisha ajali zisiwepo kabisa katika mkoa wa Tanga.

"Na kwa sasa hivi tutakuwa barabarani saa zote kuhakikisha kwamba ajali hakuna kabisa na sio kupungua,tunataka magari yaende  salama na kurudi salama,hii ndio fahari ya Tanzania tunapoona magari yanaenda salama na kurudi salama" alisema Liemba.

Amehitimisha kwa kuwataka madereva wawe makini,na yeyote mwenye matatizo amuone RTO aeleze matatizo yake na atasaidiwa kutatuliwa.

Post a Comment

0 Comments