Refa aliyekuwa akichezesha mchezo kati ya Tanesco na TRA katika mchezo wa Basketball akiwa ameshika uso wake kwa maumivu.
Refa aliyekuwa akichezesha mchezo kati ya Tanesco na TRA akitulizwa baada ya kupigwa na chupa ya maji.
Timu ya Tanesco ya Basketball imetolewa katika hatua ya nusu fainali(jana jioni) kwenye mashindano ya SHIMMUTA na timu ya TRA kwa kufungwa pointi 51-45 huku benchi la Tanesco wakimchapa mwamuzi kwa chupa ya maji kabla ya mchezo kumalizika.
Mchezo huo uliokua na upinzani ulifanyika ndani ya uwanja wa mkwakwani, uliingia dosari katika robo ya mwisho ya mchezo,baada ya benchi la ufundi la Tanesco kumpiga kwa chupa ya maji usoni mwamuzi aliyekua akichezesha mchezo huo.
Vurugu hiyo ilitokea timu ya TRA wakiwa wanaongoza kwa pointi 47-45 dhidi ya wapinzani wao Tanesco.
Wadau wa michezo waliokuwepo uwanjani hapo waliwalaumu walioanzisha vurugu hizo kwa kuwa mchezo bado ulikua upo wazi kwa pande zote mbili,kabla kuanza kwa vurugu hizo.
Wameongeza kuwa michezo hiyo inawashirikisha watumishi wa umma,sasa inapotokea uhuni kama huo kwa watumishi wa umma kupiga marefa na vyupa vya maji sijambo jema.
Fainali ya mchezo huo sasa utapigwa kati ya Bandari na TRA ambao ndio waliofuzu hatua hiyo.
0 Comments