MAFUNZO YA AWALI YA JESHI LA UHIFADHI TANAPA YAHITIMISHWA MLELE





Mafunzo ya Awali ya Jeshi la Uhifadhi kwa Wahitimu wa ajira mpya 57 wa TANAPA,yamehitimishwa jana,Mlele Katavi 28.8.2021

Mgeni Rasmi alikua Jenerali (mst) George Waitara na Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini TANAPA ambapo amesema,Mafunzo hayo yamewapa uwezo  wa usimamizi wa rasilimali za wanyamapori na misitu.

"Mafunzo yamewajengea uzalendo, uadilifu, ujasiri, utayari, kujiamini katika kulinda Maliasili za Taifa,mtapaswa kukiishi kiapo chenu cha utii kwa Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa JMT,Nendeni mkadhibiti ujangili katika maeneo ya hifadhi,mkatekeleze majukumu yenu kwa kuzingatia taratibu na miongozo yote ya Jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu"alisema Waitara.

Kwa upande wake Kaimu Kamishna wa Uhifadhi  TANAPA William Mwakilema amewapongeza kwa kuwa wa kwanza kumaliza mafunzo baada ya kusainiwa kwa kanuni na kuwa amri kuu ya Jeshi la Uhifadhi wa wanyamapori na Misitu.

"Mmekuwa kundi la kwanza kumaliza mafunzo baada ya kusainiwa kwa Kanuni na Amri Kuu za Jeshi la Uhifadhi Wanyamapori na Misitu mwezi Julai, 2021,mmeonyesha umahiri na weledi na nidhamu ya juu kwa kuanza mafunzo mkiwa 57 na kumaliza wote,nendeni mkasimamie rasilimali za wanyamapori na misitu kwa weledi mkubwa,dumisheni nidhamu katika kutekeleza majukumu yenu"alisema Kaimu kamishan Mwakilema

Shirika litaendelea kuandaa mafunzo ya mara kwa mara kuwajengea uwezo wa utendaji kazi

Pascal Shelutete
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi-Mawasiliano

Post a Comment

0 Comments