WATALII WANAONGEZEKA KILA MWAKA

 

Waziri wa Mali Asili na Utalii,Dkt.Damas Ndumbaro amesema idadi ya watalii wanaokuja nchini imekua ikiongezeka kila mwaka kutokana na Serikali kutangaza utalii.

Hayo yamebainika leo Bungeni 19/05/2021 wakati wa maswali na majibu,ambapo Mbunge Easter Bulaya alipouliza swali kutaka kujua mikakati ya kutangaza utalii

Je hamuoni kwamba ni wakati muafaka wakuwa na mikakati madhubuti ya kiushindani,ili idadi ya watalii iendane na hifadhi zetu na vivutio vyetu?

Akijibu swali hilo Waziri Ndumbaro amesema“Mh.Mwenyekiti takwimu zinaonyesha kwamba idadi ya watalii imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka,ongezeko hilo imetokana na juhudi ya Serikali ambayo imefanya katika kutangaza utalii”alisema Ndumbaro.

"Mh.Mwenyekiti ukisoma ilani ya chama cha mapinduzi imeelekeza wazi tuje na mawazo mapya ya mikakati mipya katika kutangaza utalii,Mh Mwenyekiti mikakati yote iko mezani,iko tayari kinachotukwamisha ni gonjwa la covid,ni muhakikishie Mh.Bulaya pindi ugonjwa utakapoisha ataona ongezeko kubwa la watalii"alisema Waziri Ndumbaro.

Post a Comment

0 Comments