Changamoto ya jenereta iliyokua ikiikabili uwanja wa Mkwakwani tangu ukamilike kwa ujenzi wa taa ili utumike kwa mechi za usiku umetamatika baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Tanga Rajab Abdulrahaman kutoa Shilingi Millioni Thelasini kwa ajili ya kununua jenereta la kuwasha taa za usiku katika uwanja huo uliopo jijini Tanga.
"Tunazindua taa kwa ajili ya kuja kucheza mechi,niwaombe wanatanga ule wakati tuliokuwa tukisubiri ili vilabu vya Simba,Yanga hawna haja ya kucheza mpira kwenye jua kali,kama ambavyo timu zinaenda Dar es salaam wanaambiwa mtacheza usiku,wajue kuwa safari wakija Tanga mpira utachezwa usiku"alisema Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga,Rajab.
Na katika kuhalalisha hilo,timu za Coastal Union na African Sports zitacheza mechi Februari 04,katika kutimiza miaka 46 ya Chama cha Mapinduzi CCM,katika uwanja huo ikiwa ni uzinduzi wa mechi za usiku.
Na msimamizi wa Uwanja wa Mkwakwani Naser Makau amemshukuru Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tanga,Rajab Abdulrahaman kwa kuweza kutatua tatizo la kuwaka Taa iliyokua ikiikabili uwanja huo kwa kuwa alikua akiulizwa maswali mengi,ufungaji wa taa umekamilika lakini bado haziwaki.`
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mh. Hemed Suleiman Abdullah atakua mgeni rasmi katika mchezo huo unaozihusisha timu ya Coastal Union inayotoka barabara ya 11 na African Sport inayotoka barabara ya 13.
0 Comments