ALIYEACHA UFALME ILI AOE SARAFU YAKE YA DHAHABU YAUZWA

Unaambiwa Sarafu ya dhahabu tupu yenye thamani ya pauni 5, iliyotengenezwa kwa jina la King Edward VIII,ambaye aliacha kiti chake cha Ufalme kutokana na maamuzi yake ya kuamua kuoa imeuzwa kwa bei ya rekodi.

Sarafu ya dhahabu, ambayo iliuzwa kwa pauni milioni 1,650.000 ilinunuliwa katika Mnada huko Dallas,Marekani.

Sarafu hiyo imetajwa kuwa sarafu ya gharama kubwa zaidi ya nchi ya Uingereza kuwahi kuuzwa.

Rekodi ya awali ilirekodiwa kama sarafu ya dhahabu ya pauni 5 iliyotengenezwa kwa jina la King William IV iliyotengenezwa mnamo 1831, ambayo iliuzwa huko Monaco kwa pauni 703,000.

Mfalme Edward wa 8 wa Uingereza alikua mfalme Januari 20,1936 na  aliachia madaraka mnamo mwezi Desemba 1936 ili kumuoa Wallis Simpson wa Marekani na kuhamisha makazi yake nchini Ufaransa.

Baada ya uamuzi huo, madaraka yalienda kwa kaka yake George ambaye alitawazwa kuwa mfalme Mwezi Mei,1937.

Edward VIII,siku yake ya Harusi akiwa na mke wake Wallis Simpson 3 June 1937 huko Chateau de Cande,nchini Ufaransa.

Post a Comment

0 Comments