MGOMBEA UBUNGE TANGA MJINI,UMMY MWALIMU:BIMA YA AFYA ITAWAKOMBOA WANANCHI .


Mgombea ubunge jimbo la Tanga mjini, Ummy Mwalimu akizungumza na wananchi wa kata ya Ngamiani Kaskazini wakati akinadi sera zake na Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM 06/10/2020.
Hapo vipii..mgombea ubunge Jimbo la Tnga Mjini Ummy Mwalimu wakati akinadi sera za Chama cha Mapinduzi katika mkutano wake uliofanyika 06/10/2020 katika kata ya Ngamiani Kaskazini.

Mgombea Ubunge jimbo la Tanga Mjini,Ummy Mwalimu akipanda jukwaani kunadi sera kwenye mkutano wake aliofanyia katika kata ya Ngamiani Kaskazini,06/10/2020.

Mgombea Ubunge jimbo la Tanga Ummy Mwalimu amesema Serikali itaendelea kuboresha huduma za Afya katika kipindi cha 2020-2025 katika ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa kuboresha Bima ya Afya.

Ummy ameyasema hayo akiwa katika kata ya Ngamiani Kaskazini wakati wa kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwaongoza wananchi jimbo la Tanga.

"Tunaahidi katika ilani kuboresha huduma za afya kwa kuwa changamoto kubwa ni gharama za matibabu,hivyo serikali imeamua kuboresha Bima ya Afya ili watanzania wote wenye fedha na wasio na fedha wanapata huduma bila kikwazo cha fedha,Rais Magufuli amelisema sana na mimi kama waziri wake tutalifanyia kazi,suala bima ya Afya ili watu wote wapate huduma".

Katika hatua nyingine amesema kituo cha Afya Ngamiani bado itaendelea kuboresha huduma zake na itaendelea kutoa huduma kwa kina mama wajawazito,watoto na wazee wanapata huduma bila malipo.

Aidha Ummy amewataka wananchi wachague viongozi wanaoweza kuleta maendeleo na sio kuwachagua watu waliofilisika kisiasa, hawana hoja.

"Tunatafuta mbunge,mnatafuta mtu wa kuwasimamia wa kwenda kupiga hopdi wa kwenda kupiga hodi kwa viongozi wakuu wa nchi,wakutafuta wawekezaji msifanye makosa Tanga mjini,msifanye makosa kwa maneno ya uongo kwa maneno ya uzushi,nina simama kwa sababu ya uwezo wangu".

Kwa upande wa Elimu amesema atahakikisha kunakuwa na mazingira mazuri kwa wanafunzi na  kwa walimu ili waweze kufanya kazi katika mazingira ya kumwezesha mwanafunzi kufanya vizuri katika masomo.








Msanii Kassim Mganga alikuwepo kuburudisha wananchi waliojitokeza


Post a Comment

0 Comments