Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amepiga picha ya pamoja na viongozi wa Diaspora ya Tanzania nchini Ethiopia mara baada ya kukamilisha ziara yake ya kikazi, Februari 15, 2026.
Katika ziara hiyo ya siku nne, Rais Dkt. Samia alishiriki katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Februari 14 na 15, 2026, ambapo viongozi wa bara la Afrika walikutana kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, usalama na ushirikiano wa kikanda.
Mbali na kushiriki mkutano huo, Rais Dkt. Samia alipata fursa ya kukutana na Watanzania wanaoishi nchini Ethiopia, akisisitiza umuhimu wa Diaspora kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Taifa pamoja na kuendeleza diplomasia ya uchumi.

0 Comments