Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba Aongoza Kikao Kujadili Maboresho ya Sheria ya Mapato

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Machi 11, 2026, ameongoza kikao cha kujadili mapendekezo ya kufanya maboresho ya Sheria ya Mapato ya baadhi ya Mifuko. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Waziri Mkuu, Bungeni jijini Dodoma.

Baadhi ya viongozi walioshiriki katika kikao hicho ni pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) William Lukuvi, Waziri wa Ujenzi Abdallah Ulega, Waziri wa Fedha Balozi Khamis Mussa Omar, Waziri wa Madini Anthony Mavunde, na Waziri wa Nishati Deogratius Ndejembi.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Wanu Hafidh Ameir, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Ummy Nderiananga, Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) Dkt. Jim Yonaz, pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha Dkt. Natu El-Maamry.

Post a Comment

0 Comments