Bodi ya Wadhamini Shule ya Uongozi Mwalimu Nyerere Yakutana Chini ya Uongozi wa Dkt. Migiro

 


Makatibu Wakuu wa Vyama Rafiki vya Ukombozi Kusini mwa Afrika, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Asha-Rose Migiro, wameshiriki katika Kikao cha Bodi ya Wadhamini wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere (MJNLS) kilichofanyika tarehe 4 Machi 2026 mjini Kibaha, mkoani Pwani.

Wajumbe wengine waliohudhuria kikao hicho ni Katibu Mkuu wa Chama cha ANC (Afrika Kusini), Fikile Mbalula; Katibu Mkuu wa Chama cha FRELIMO (Msumbiji), Chakil Felizardo Passadas Aboobacar; na Katibu Mkuu wa Chama cha ZANU-PF (Zimbabwe), Jacob Francis Nzwidamilimo Mudenda.

Aidha, Chama cha SWAPO (Namibia) kiliwakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dkt. Samuel Abraham Peyavali Mushelenga, huku Chama cha MPLA (Angola) kikiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Frederico Toth Jorge De Miranda.


Post a Comment

0 Comments