Akizungumza wakati wakifanya zoezi hilo Afisa madai NHIF Tanga,Petro Aloyce ameeleza huduma ambazo zinapatikana kwenye Mfuko wa Bima ni kupitia vifurushi ambavyo vimegawanyika kupitia umri kwa mwanachama anayehitaji ili kumfikia mtanzania mmojammoja ambazo ni NAJALI AFYA,WEKEZA AFYA na kifurushi cha TIMIZA AFYA.
"Hivi vifurushi vimegawanyika kwenye garama kulingana na umri wa mwanachama na wigo wa matibabu ambao mwanachama anahitaji kupata kwa wakati huo"Alisema.
Moja ya elimu waliyoitoa ni Bima ya Toto Afya Kadi kwa watoto walio chini ya Umri wa miaka 18 ambayo ni Shilingi 50400 kwa mtoto mmoja kwa mwaka mzima.
Aidha ameongeza kuwa kuna vifurushi vya wajasiriamali BODABODA AFYA,MAMA LISHE na CHINGA AFYA,ambavyo vinatolewa kwa misingi ya wanachama kuwa katika makundi maalum.
"Hivi vyote tunatoa kwa misingi ya kwamba wahusika wawe katika makundi yaliyosajiliwa na yanayotambulika kisheria"Alisema
Hata hivyo amesema zoezi hilo ni moja ya shughuli zao kuhakikisha wananchi wanapata elimu ya bima na kuifahamu kwa undani zaidi.
Wafanyakazi wa mfuko wa Bima ya Afya Petro Aloyce pamoja na Ezekiel Enock wakiwa mtaani kutoa elimu kuhusu umuhimu wa Bima.
0 Comments