RAIS MHE.SAMIA SULUHU AIAGIZA TAKUKURU KUANDAA MIFUMO NA MIKAKATI MIPYA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akielekea katika ukumbi wa Mikutano wa Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma kwa ajili ya kupokea Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG kwa mwaka wa Fedha 2019/2020 leo tarehe 28 Machi 2021


Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Charles Kichere akionesha moja ya Taarifa zake za ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/20 kabla ya kuziwasilisha kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo tarehe 28 Machi 2021 katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20  Bw. Charles E Kichere Ikulu Chamwino Jijini Dodoma leo March 28,2021.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Brigedia Jenerali John Mbungo wakati akitolea Maelezo moja ya Taarifa yake ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa kwa mwaka 2019/20


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokea Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020 kutoka kwa Mkuu wa Taasisi hiyo Brigedia General John Mbung’o leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Naibu Spika Mhe.Tulia Akson baada ya kumalizika kwa Hafla ya upokeaji wa Taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG za mwaka wa fedha 2029/20 na Taarifa ya Taasisi ya Kuzuwia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ya mwaka 2019/2020  leo March 28,2021 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma. (Picha na Ofisi ya Rais)

************************

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuandaa mfumo madhubuti wa kupambana na Rushwa kwani vitendo hivyo bado vinaendelea katika maeneo mbalimbali.

Ameyasema hayo leo mara baada ya kupokea taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) pamoja na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Ikulu Jijini Dodoma.

“Serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya vitendo vya Rushwa kwani vitendo hivyo vimezidi kuendelea hivyo ni lazima kuwe na mikakati na mifumo mipya ya kukabiliana navyo”. Amesema Rais Mhe.Samia Suluhu.

Aidha Mhe.Samia amesema atasimama imara katika mapambano dhidi ya Rushwa hasa Rushwa ya ngono ambayo imekidhiri katika maeneo mengi.

Pamoja na hayo amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Dr. Charles Kichere kutokuwa na kigugumizi chochote kwenye Shirika analoona halifanyi vizuri kimapato.

“Tukinyamaziana kwa kutazamana sura hatutarekebisha na tutawaumiza Wananchi, naomba sana ripoti yako CAG iwe wazi zaidi, utakaponiletea ukaguzi wa Mashirika naomba uwe wazi zaidi ili tujue tunachukua hatua gani”.Ameeleza Rais Mhe.Samia Suluhu.

Post a Comment

0 Comments