MADAKTARI KENYA WAGOMA.

Serikali ya Kenya kupitia Waziri wake wa Afya Mutahi Kagwe imetishia kuwafuta kazi madaktari na wahudumu wa hospitali za umma nchini humo walioamua kugoma.

Madaktari nchini Kenya wanaofanya kazi kwenye hospitali za umma wameungana na wahudumu wengine kwenye mgomo kwa kutopewa bima ya afya na kufanya kazi kwenye mazingira magumu hasa katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linapitia changamoto ya janga la virusi vya Covid-19.

Mgomo huu unakuja baada ya mazungumzo kati ya wawakilishi wa Madaktari na Serikali nchini humo kugonga mwamba.

Kufikia sasa Kenya imerekodi visa 94,614 vya maambukizi ya virusi vya Corona baada ya visa vipya 114 kuthibitishwa na vifo 1,644 baada ya ya watu wengine 5 kuthibitishwa kufariki dunia kutoka na janga hilo hatari la COVID-19.

Ripoti kutoka nchini Kenya zinaonyesha kuwa taifa hilo la Afrika Mashariki limeendelea kupoteza wahudumu wa sekta ya afya wanaoaga dunia kutokana na Covid-19.

Wananchi wa Kenya wamekasirishwa na ongezeko la vifo vinavyotokana na janga la corona hasa miongoni mwa wahudumu wa afya baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita,madaktari wawili maarufu nchini humo kupoteza maisha, huku wahudumu wa afya zaidi ya 1,000 wakiwa wameambukizwa.

Post a Comment

0 Comments