PUTIN NA XI JINPING WASUSA MKUTANO WA G20

Mkutano wa mataifa tajiri na yenye uwezo kiuchumi unaanza rasmi leo Jumamosi Jijini New Delhi nchini India. 

Baadhi ya viongozi wameelekea huko akiwemo Rais wa marekani Joe Biden wakati huu kukiwa na taarifa kuwa viongozi wa China na Russia hawatahudhuria mkutano huo.

Hapo siku ya Alhamisi taarifa ya Kremlin ilisema kuwa rais wa Urusi hana nia yashiriki mkutano huo au hata kuhudhuria kwa njia ya vídeo. Rais wa China Xi Jinping pia hatahudhuria mkutano huo.

Rais wa Marekani Joe Biden anatumai kutumia nafasi ya kukosekana kwa viongozi hao wawili , Xi Jinping  na Putin ili kuimarisha ushawishi wa Washington.

Viongozi hao wanakutana wakati huu kukiwa na mgawanyiko mkubwa kufuatia  vita vya Ukraine na jinsi ya kuyasaidia mataifa yanayoinukia kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi. Juzi tuu marekani iliipa msaada wa ndege zisizo na rubani nchi ya Ukraine. Swala ambalo urusi ilisema ni kinyume na ubinaadamu.

Katika miaka ya hivi karibuni, bara la Afrika limealikwa kwa utaratibu kwenye mikutano ya kilele ya kundi hili. Mwaka huu, uwepo wake ni muhimu zaidi kuliko wakati mwingine wowote kwa kuzingatia majanga mengi yanayoathiri Afrika, iwe uhaba wa chakula, hali ya hewa, nishati au madeni

Post a Comment

0 Comments