RAIS DKT.SAMIA AAGIZA HUDUMA ZA DHARURA MAENEO YALIYOATHIRIWA NA KIMBUNGA HIDAYA


RAIS Dkt. Samia Suluhu Hassan ameagiza huduma za dharura zipelekwe kwenye maeneo yaliyopata athari kutokana na kimbunga Hidaya.

Hayo yamesemwa leo (Mei 6, 2024) na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye kikao cha dharura cha Kamati ya Maafa Kitaifa alichokiitisha kupokea taarifa ya hatua zilizochukuliwa kwenye maeneo yaliyopata athari.

“Rais ameelekeza hatua za haraka zichukuliwe katika maeneo yote yaliyoathiriwa na mvua zilizotokana na athari za kimbunga Hidaya ikiwa ni pamoja na kupeleka misaada,” amesema. Maeneo yatakayopelekewa misaada hiyo ni Mafia mkoani Pwani, Kilwa (Lindi) na Ifakara (Morogoro).

Mkuu ameliagiza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lihakikishe linakamilisha zoezi la uokoaji katika maeneo ya Kilwa ambapo zaidi ya kaya 40 zimezingirwa na maji. “Jeshi la Zimamoto mmefanya kazi kubwa, hakikisheni maeneo yenye makazi yaliyozingirwa na maji, wakazi wake wanaondolewa na kupelekwa maeneo salama pamoja na kupewa huduma zote muhimu.”

Post a Comment

0 Comments