TMA INAENDELEA NA UDHIBITI NA URATIBU WA MUFUMO YA HALI YA HEWA

Moja ya mitambo mipya ya Rada iliyofungwa na Mamlaka ya hali ya Hewa TMA kupitia serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

************

Katika kuhakikisha wananchi wanaishi katika hali ya utulivu pamoja na mali zao na kuchukua tahadhari mbalimbali katika majanga yanayoweza kujitokeza kutokana na hali mbaya ya hewa Serikali kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea na utoaji wa huduma, kudhibiti na kuratibu shughuli za hali ya hewa hapa nchini. 

Akiwasilisha Bajeti ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi kwa mwaka 2024/2025 Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa amesema  TMA imeendelea kutoa huduma za utabiri wa kila siku, siku kumi na ule wa muda mrefu pamoja na tahadhari ya matukio ya hali mbaya ya hewa ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao ambapo usahihi wa utabiri umefikia asilimia 86 ambao ni juu ya asilimia 70 ya kiwango cha usahihi kinachokubalika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO).

Waziri Profesa Mbarawa ameongeza kuwa TMA ilifanyiwa ukaguzi wa kimataifa kuanzia tarehe 22 – 27 Januari 2024, na kuendelea kukidhi vigezo vya kumiliki cheti cha ubora (ISO 9001: 2015).

“Katika kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2020 Ibara ya 59(j) na Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano (FYDP III 2021/22-2025/26), Serikali iliahidi kuendelea kuimarisha miundombinu na huduma za hali ya hewa ikiwemo ununuzi wa rada,” Amesema Profesa Mbarawa

Amelitaarifu Benge kuwa  Serikali kupitia TMA imekamilisha ufungaji wa rada za hali ya hewa katika mikoa ya Kigoma na Mbeya na kufikisha jumla ya rada tano (5) za hali ya hewa nchini.

Post a Comment

0 Comments