Katika kuhakikisha kuwa shughuli za kilimo na ufugaji na shughuli nyinginezo zinazotekelezwa na vyama vya ushirika zinakuwa endelevu na salama,vyama hivyo vimeshauriwa kukata bima kwa ajili ya kulinda shughuli hizo dhidi ya majanga mbalimbali.Aidha,vyama hivyo vimeshauriwa kujisajili kama watoa huduma za bima ili kujiongezea kipato.
Ushauri huo umetolewa na Meneja wa Kanda ya Kaskazini Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Bahati Ogolla, wakati wa Jukwaa la Saba la Maendeleo ya Vyama vya Ushirika lililofanyika Mkoa wa Tanga tarehe 4 Juni,2025.
Ogolla amesema kuwa vyama vya ushirika vina nafasi kubwa ya kununua bima kwa ajili ya kukinga majanga mbalimbali yanayoweza kujitokeza katika shughuli zao za kila siku mfano kilimo na ufugaji.
"Kuna bima mahususi kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo ambazo vyama vinaweza kuzinunua ili kujikinga na vihatarishi vinavyoweza kuathiri mazao au mifugo yao"alisema Ogolla.
Aidha,alibainisha kuwa SACCOS zinazotoa mikopo kwa wanachama wao zinaweza pia kunufaika na bima ya mikopo, ambayo hutumika kama mbadala wa dhamana kwa wanachama wanaokopa.
0 Comments