MELI ZA CONTENA ZAGONGANA CHINA.

Watu 3 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali ya meli mbili zilizogongana katika Mto Yangzi unaopita mji wa Shanghai nchini China.

Meli hizo mbili za makontena zinazoitwa "Oceana" na "Xinqisheng 69", ziligongana katika eneo ambalo mto unatiririkia kwenye Bahari ya Mashariki ya China.

Kwa mujibu wa taarifa za China Daily, meli ya Xinqisheng 69, yenye urefu wa mita 165 na iliyokuwa imebeba makontena 650, ilipinduka baada ya ajali hiyo ya mgongano.

Watu 3 wameripotiwa kupoteza maisha kutokana na ajali ya meli mbili zilizogongana katika Mto Yangzi unaopita mji wa Shanghai nchini China.

Timu ya uokoaji iliwawaokoa wafanyakazi 8 kati ya 16 waliokuwemo kwenye meli, na kupata maiti za watu 3 na shughuli ya utafutaji wa watu wengine 5 waliopotea bado inaendelea

Post a Comment

0 Comments