UTATA WA CHANJO YA AstraZeneca ya UINGEREZA

Watu 7 waliopewa chanjo ya Oxford-AstraZeneca iliyozalishwa dhidi ya corona (Covid-19) nchini Uingereza wameripotiwa kufariki kutokana na tatizo la kuganda kwa damu.

Kati ya watu milioni 18.1 nchini humo ambao walipewa chanjo ya Oxford-AstraZeneca, 30 walikumbwa na tatizo la kuganda kwa damu.

Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Dawa na Huduma za Afya nchini Uingereza (MHRA), watu 7 kati ya hao 30 walifariki.

Kwa mujinu wa mamlaka ya MHRA,  hadi kufikia sasa hakuna ushahidi wowote unaoonyesha uhusiano kati ya kuganda kwa damu na chanjo ya Oxford-AstraZeneca.

Uchunguzi bado unaendelea ili kubainisha iwapo kuna uhusiano wowote kati ya vifo na chanjo, au vifo hivyo vimetokea kwa bahati mbaya.

Kati ya tarehe 9 Desemba na 21 Machi, dozi milioni 15.8 za kwanza za chanjo ya Oxford-AstraZeneca zilitolewa na dozi milioni 2.2 za pili zikatolewa nchini humo.

Baadhi ya nchi za Ulaya zimesitisha matumizi ya chanjo hiyo au kupunguza utumiaji wa chanjo hiyo kutokana na madai ya kusababisha  tatizo la kuganda kwa damu.

Post a Comment

0 Comments