WFP:KENYA KUKABILIWA NA BAA LA NJAA

Shirika la Mpango wa Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) limetangaza kuwa, watu milioni 2.4 wapo katika hatari ya kukabiliwa na baa la njaa nchini Kenya kufikia mwezi Novemba mwaka huu.

Taarifa ya WFP inasema kuwa, hali inatarajiwa kuwa mbaya,mara tatu zaidi  ikilinganishwa na hali ilivyokuwa mwaka uliopita (2020), wakati watu 852,000 waliporitiwa kukabiliwa na baa la njaa nchini Kenya.

Taarifa zinaonyesha kuwa, maeneo ya kaskazini na mashariki mwa Kenya yanaendelea kukabiliwa na ukame.

Shirika hilo licha ya kuomba msaada wa dola milioni 139 kusaidia kukabiliana na majanga kama haya, lakini mpaka sasa ni dola milioni 28 tu ndizo zilizopatikana kutoka kwa wahisani.

Katika miaka ya hivi karibuni taifa hilo la Afrika Mashariki limekabiliwa na majanga kama uvamizi wa nzige mwaka 2019, lakini pia ukosefu wa mvua ya kutosha kati ya mwaka jana (2020) na mwaka huu.

Mwezi Septemba,Rais Uhuru Kenyatta alitangaza ukame kama  janga la kitaifa huku mamilioni ya watu  wakiendelea kukabiliwa na baa la njaa na kueleza kuwa serikali yake imetenga dola milioni 18 kuwasaidia wanaoathirika.

Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa FAO linasema Kenya imepiga hatua kubwa katika kudhibiti nzige wa jangwani ambao walivamia eneo la Afrika Mashariki mapema mwezi February na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazao. 

Uvamizi huo wa nzige ulihatarisha maisha ya mamilioni ya watu na uhakika wa chakula baada ya mazao kuharibiwa.

Post a Comment

0 Comments