TPA WATOA VIFAA TIBA KITUO CHA AFYA MAKUYUNI

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Nchini(TPA)Mkoa wa Tanga imetoa msaada wa vifaa tiba pamoja na viti mwendo(wheel chair)vyenye thamani ya sh.Mil 10 kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma katika kituo cha Afya ya Makuyuni.

Msaada huo ambao ni kwa ajili ya maadhimisho ya wiki ya Bandari,uzinduzi huo umefanyika kwenye Kituo cha Afya Makuyuni iliyopo wilayani Korogwe.

Meneja Bandari ya Tanga Masoud Mrisha amsema kuwa msaada huo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii sehemu ya faida ambayo wameipata katika kipindi Cha mwaka mzima cha utoaji wa huduma za bandari.

Akiongea wakati wa kupokea msaada huo Mkuu wa wilaya ya Korogwe Joketi Mwigelo amesema kuwa dhamira ya serikali ni kuona wananchi wake wanapata huduma za afya zenye ubora lakini karibu na maeneo yao.


MKUU wa wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo kushoto akipokea msaada wa vifaa tiba wenye thamani ya Milioni 10 kutoka kwa Meneja wa Bandari ya Tanga Masoud Mrisha kwa ajili ya Hospitali ya wilaya ya Korogwe ikiwa leo ni siku yao ya kusheherekea kuanzishwa kwa Mamlaka ya Bandari nchini.

Post a Comment

0 Comments