Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika UNESCO, Saidi Othman Yakubu, ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii kwa juhudi inazofanya katika kuhifadhi Maeneo ya Urithi wa Dunia pamoja na kutumia rasilimali hizo kukuza utalii na uchumi wa Taifa.
Balozi Yakubu ametoa pongezi hizo Agosti 31, 2026, alipokutana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Hassan Abbasi, kufuatia ziara yake ya kikazi iliyofanyika Agosti 14 hadi 28, 2026, katika maeneo mbalimbali ya Tanzania.
Katika ziara hiyo, Balozi Yakubu alitembelea maeneo ikiwemo Kondoa, Ngorongoro, Serengeti, Kilimanjaro, Kilwa, Zanzibar na Selous, kwa lengo la kujionea hali ya uhifadhi pamoja na fursa zilizopo katika maeneo hayo.
Amesema ziara hiyo imemwezesha kuona mafanikio yaliyopatikana katika uhifadhi na kubaini fursa zaidi za kuongeza idadi ya watalii, uwekezaji, ajira na mapato ya Taifa.
Aidha, pande hizo zimekubaliana kuimarisha ushirikiano na kutumia diplomasia ya utalii katika kuitangaza Tanzania kimataifa na kuongeza fursa za kiuchumi kupitia sekta ya utalii.


0 Comments