Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi,Uenezi na Mafunzo,Kenan Kihongosi anatarajiwa kufanya ziara ya siku mbili katika Wilaya za Mkinga na Tanga Mjini, mkoani Tanga.
Katika ziara hiyo, Kihongosi anatarajiwa kukutana na wananchi kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzitafutia ufumbuzi, pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Tanga na nyumba za viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akizungumza kuhusu ziara hiyo Katibu wa Itikadi,Uenezi na Mafunzo wa CCM Wilaya ya Tanga,Kipanga Salim amesema Kihongosi anatarajiwa kuwasili mkoani Tanga Septemba 25, 2026,ambapo ataanza rasmi ziara hiyo ya siku mbili.

0 Comments