Naibu Waziri wa Maji Kundo Methew ataka vyanzo vya maji kulindwa dhidi ya El Nino

Naibu Waziri Wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amezitaka Mamalaka Za Maji Mkoani Manyara Ikiwemo RUWASA na Mamlaka ya maji mji wa Babati -BAWASA kuamarisha Ulinzi Wa Vyanzo Vya Maji Dhidi ya athari za Mafuriko na Uchafuzi katika Kipindi Cha Mvua Za Elnino zilizotabiria na Mamlaka ya hali ya hewa nchini TMA. 

Mhandisi Kundo Mathew ametoa maelekezo hayo wilayani Babati mkoani Manyara katika Ziara Yake Ya Kukagua Mradi wa Maji ya Darakuta hadi Minjingu Unaotekelezwa kwa BAWASA na Mradi Wa Maji Wa Kijiji Cha  Ayasanda Unaotekelezwa na RUWASA. 

Katika ziara hiyo Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Kundo Mathew amesisitiza Mamlaka za maji mkoani Manyara kutoa elimu Kwa Wananchi kuhusu madhara ya tabia ya baadhi ya watu Kufungulia hovyo mifumo ya Maji Taka wakati wa mvua ili Kuepusha kutokea magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu. 

Pia ameelekeza kuundwa kwa timu maalum ya kutatua haraka changamoto za maji wakati mvua za El nino.

Kwa Upande Wake Katibu Tawala Wilaya Ya Babati Thobias Abwaro ameiomba Serikali Ikamishe ujenzi wa  Miundombinu ya bwawa la kuhifadhi Maji Taka uliosimama kwa takribani miaka mitano sasa.

Awali akitoa taarifa Ya Hali Ya Upatikanaji Wa Maji Katika Mkoa Wa Manyara ,Meneja Wa Ruwasa Mhandisi James Kionaomela amesema uwekezaji mkubwa uliofanywa na serikali mkoani Manyara umewezesha Wastani Wa Upatakanaji Wa Maji kimkoa kufikia asilimia 86.

Post a Comment

0 Comments