Wasaidizi wa kisheria mkoa wa Tanga wapewa Elimu ya kujikinga COVOD 19


Wasaidizi wa kisheria mkoani Tanga wamepewa mafunzo ya kuwasaidia watu ndani ya jamii juu ya hatua za  kujikinga na ugojwa wa COVOD 19.

Akizungumza mratibu wa shirika la TEWOREC mkoani Tanga Halima Saguti amesema kuna haja kubwa ya kuwajenga kiuwezo wasaidizi wa kisheria kutoka halimashauri 11 za mkoani hapa.

Saguti amesema licha kuwepo kwa ugonjwa wa COVOD 19 na vitendo vya ukatili wa kijinsia unaendelea na unahitajika kutokomezwa kwa hali ya juu ndiyo maana mafunzo haya yamewafikia watetezi wa kisheria katika jamii.

Kwa upande wake kaimu afisa Afya wa jiji la Tanga Hamza Maulidi amesema mafunzo hayo yamewalenga maafisa hao kwa wakati muwafaka kwani washiriki wote wamafunzo hayo watafundishwa kutengeneza vitakasa mikono(sanitaizer) kwa manufaa ya jamii inayowangunguka.

Nao baadhi ya washiriki akiwemo Maria Senga amesema mafunzo hayo yamewasaidia kuongeza kasi ya kusaidia jamii katika maswala ya kisheria na kuwaondolea hofu watanzania juu ya uwepo wa ugonjwa wa COVOD 19 na kuwataka wazingatie kanuni za kiafya

Post a Comment

1 Comments

  1. Vizur mlezi wetu mungu akupe kher ktk mambo yako we p1 na jopo zima la TEWOREC

    ReplyDelete