SUDAN WAGOMA KUREJEA MAZUNGUMZO KUHUSU UJENZI WA BWAWA UNAOFANYWA NA ETHIOPIA.

Serikali ya Sudan imetangaza kukataa kurejea katika meza ya mazungumzo kuhusu mzozo wa Bwawa la al-Nahdha unaoendelea kufanywa na Ethiopia.

Sudan imetangaza kuwa,nchi hiyo haiko tayari kurejea katika mazungumzo hayo katika mazingira ya hivi sasa.

Taarifa ya Sudan imeeleza kuwa,licha ya Ethiopia kutangaza kuendelea mazungumzo kuhusu Bwawa la al-Nahdha kuanzia Jumatatu ya leo, lakini Khartoum haiko tayari kurejea katika mazungumzo hayo.

Sudan imesisitiza kuwa, itarejea katika mazungumzo hayo pale Ethiopia itakapofungamana na makubaliano yaliyofikiwa hapo kabla.

Hata hivyo Serikali ya Ethiopia imetangaza kuwa, haiko tayari kutia saini makubaliano ambayo yanaainisha hisa maalumu kwa nchi za Ukanda wa Mto Nile.

Hayo yanatokea baada ya Spika wa Bunge la Misri Ali Abdul-Aal,kueleza kusikitishwa kwake na msimamo wa serikali ya Ethiopia aliutaja kuwa ‘usio wa ushirikiano’ kuhusiana na kadhia ya Bwawa la al-Nahdha.

Ujenzi wa Bwawa la  Renaissance (al-Nahdha) unaofanywa na Ethiopia juu ya maji ya Mto Nile tangu mwaka 2011 umezusha mvutano mkubwa baina ya nchi tatu za Misri, Sudan na Ethiopia.

Misri na Sudan zina wasiwasi kwamba ujenzi wa bwawa hilo utapunguza mgao wao wa maji na kusababisha tatizo kubwa la maji katika nchi hizo. Hadi sasa kumefanyika duru kadhaa za mazungumzo baina ya wawakilishi wa nchi hizo tatu lakini hayajakuwa na matokeo mazuri na ya kuridhisha.

Chanzo Pars.

Post a Comment

1 Comments

  1. Je unahitaji nyumba ya kifahari ya kununua? Nyumba ipo bunju ukubwa wa kiwanja sqm 1860 nyumba ina hati je nyumba ikoje? Nyumba ya gorofa ina vyumba vitano vyote self ina nyumba ndogo pembeni ina bwawa la kuogelea swimming pool inagadeni bustani kubwa sana inamiti ya matunda bei yake sio mbaya kutoka barabara ya bagamoyo kuifata nyumba ni klm mbili tu nipigie simu kwa namba hii +255713418477 naitwa john nauza kwa niaba ya.

    ReplyDelete