Dunia inakwenda kasi sana,unapowasha simu yako na kufungua programu ya WhatsApp kuna maelezo yanakuja..sasa basi kuanzia mwezi Februari watatakiwa kufuata masharti yanayotolewa lasivyo hautaweza kutumia WhatsApp tena.
WhatsApp inabadili vigezo na masharti (terms) zake na sera ya faragha (privacy policy) kwa watumiaji wake wote kuanzia Februari 8.
Watumiaji wote wa WhatsApp ambao ni zaidi ya Billion 2 duniani wanalazimika kukubaliana na kanuni na vigezo vipya au kufutiwa account ya WhatsApp moja kwa moja.
Katika notification ambayo inatokea kwenye WhatsApp, haijasema kiundani kuhusu mabadiliko mapya lakini imesema WhatsApp itaanza kukusanya taarifa ili kuelewa matumizi ya watumiaji wake, na itatumia taarifa hizo kuboresha app na kutumika katika mipango ya Facebook.
WhatsApp imesema ni lazima ikusanye taarifa za watumiaji wake ili kuendesha, kutoa, kuboresha, kuelewa, na kukuza huduma zake, pamoja na Facebook.
Pia WhatsApp imesema itatumia taarifa hizo katika platform zote za Facebook na wadau wengine (Third-parties) kufanya maboresho na kutumia data za watumiaji kufanya maboresho.
Pia WhatsApp imesema itatumia taarifa hizo katika platform zote za Facebook na wadau wengine (Third-parties) kufanya maboresho na kutumia data za watumiaji kufanya maboresho.
Japo haijasema ni taarifa zipi itakuwa inazikusanya na kuzitumika katika platforms za Facebook lakini imesema ni lazima kukubali na mwisho ni February 8, ukikataa inafuta account yako moja kwa moja.
0 Comments