GOSPEL PRINCES KUJA KITOFAUTI

Muimbaji wa nyimbo za injili mkoani Tanga Cesy Bunto maarufu kwa jina la Gosple Princes amesema licha ya ukimya uliopo kwa sasa amepanga kuwafanyia supprice wapenzi na mashabiki wake kwa kuachia video ya aina yake ambayo anaamini  itawaacha vinywa wazi mashabiki na wapenzi wa kazi yake.

Amesema kukaa kimya kwa muda mrefu haimaanishi kuwa hafikirii tena kuhusiana na mziki huo licha ya  kumekuwa na maneno ya hapa na pale yakimhusisha msanii huyo kuachana na huduma hiyo ya uimbaji.

Wimbo wa mwisho  kuuachia mwaka jana 2020 mwanadada huyo umekwenda kwa jina la UWEPO na alisema kutokuachia nyimbo nyingine ni kutokana na watuambao wanampa company ambao wamemshauri lakini anarejea na makali yaleyale.

"Najua wengi wanajiuliza kwanini nipo kimya tangu nilivyoachia wimbo wa mwisho lakini wapo watu wa karibu ambao wananishauri na kunipa ushirikiano wao ndio wamenifanya kuwa hivyo lakini sio kwa ubaya ni ili kitaka nitoe vitu bora zaidi" alisema Gospel princes

Anajua mashabiki wake wanataka nini ambapo  wengine wanajiuliza kuhusiana na ukimya huo wa muda mrefu hivyo  kukiri kuwa  majibu ya maswali yao yanakuja hivi karibuni kupitia video mpya ambayo ipo tayari na anasubori tu mida ufike.

Gospel Princess alisema kamwe mahusiano hayawezi kuingilia kazi yake ya uimbaji  kwani anaamini ni wito ambao ameitiwa na Mungu hivyo yuko tayari kuvunja mahusiano yake ya  kimapenzi na mtu yeyote ambaye hatomsupport kwa kile anachokifanya.

"Napenda Sana kuimba nmechagua njia hii kumtumikia Mungu na nmeahidi kumtumikia maisha yangu yote" alisema  Gosper princess.

"Namuomba sana Mungu anipatie mtu ambaye atathamini kile ambacho nakifanya, sipo tayari kuwa na mtu ambaye ataniweka mbali na Mungu."alisema.

Mbali na uimbaji Gosper Princes anajishughulisha na ujasiriamali lakini pia ni mtangazaji vitu ambayo vinazidi kumtanulia wigo wa kutengeneza mashabiki wengi.

Post a Comment

0 Comments