Akizungumza katika uzinduzi wa kituo hicho mchunguzi wa lugha kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA) Anold Msofe alisema serikali inatambua mchango wao katika kuunga mkono juhudi za kukuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi ambapo amebainisha kuwa baraza limeandaa miongozo itakayowawezeaha walimu kufundisha kiswahili fasaha.
"Sisi kama walezi wa kiswahili baraza na serikali tunalipongeza shirika hili la SUUKI kwa hatua waliyochukuwa hii ni faraja kwetu kuona vituo vinaongezeka ndani na nje ya nchi kwa lengo la kukuza lugha yetu, BAKITA tuko nao bega kwa bega katika jitihada za kuendelea kukuza kiswahili" alisema Msofe.
Hata hivyo Msofe ametoa rai kwa watanzania wenye kutaka kufungua vituo vya kufundishia lugha ya kiswahili katika maeneo mbalimbali hapa nchini kufuata utaratibu uliowekwa na BAKITA kuhakikisha maendeleo ya lughaambapo alisema kila mmoja anayo haki na wajibu wa kufungua kituo cha kufundishia ili kuisaidia serikali katika jitihada zake za kueneza lugha ya kiswahili .
"Sasa hivi kiswahili ni bidhaa adimu tanapenda kuona kuona mila mmoja anawajibika katika hili, ni vizuri ukafahamika na Bakita, usifundishe tu kinyemela, tunafanya haya ili wageni wakija waone nchi ina utaratibu wake lakini wasipate usumbufu." alisema Msofe.
Kwa upande wake mkurugenzi wa shirika la urithi wa utamaduni wa kiswahili (SUUKI) mkoa wa Tanga Bw. Joseph Gasper ameipongeza serikali kwa jitihada inazozifanya za kukuza kiswahili huku akiiomba kwa kishirikiana na BAKITA kuweka Sera rafiki zitakazoweza kukuza kiswahili nchini.
" Kuna changamoto mbalimbali katika lugha yetu mfano mpaka sasa hakuna sera rasmi ya kukuza lugha ya kiswahili niombe serikali pamoja na bakita kuangalia kwa makini katika hili, kumekuwa na mabadiliko ya matamko ya sera mbalimbali juu ya lugha ya kiswahili ile hali ya kupuuza lugha ya kiswahili tungependa kwanza iondokane na viongozi wa juu ndio wanachi wa kawaida wataweza kuona umuhimu wa ustawi wa lugha yetu" alisema Bw Gasper.
Aidha mkurugenzi Huyo alisema kuwa endapo kiswahili kitaendelea kupewa kipaumbele kitazidi kufungua fursa za maendeleo hapa nchini kwa kuvutia wageni kutoka nje ya Tanzania kupitia sekta ya utalii.
"Ni ngumu Sana kupata huduma kama utaenda sehemu ambayo hujui tamaduni za sehemu husika, tunapata watalii wengi ambao wanakuja kujionea mambo mbalimbali ni matumaini yangu kama kiswahili kitafundishwa kwa ufasaha tutazidi kupata wageni wengi zaidi" aliongeza.
Nao baadhi ya walimu wa kiswahili kutoka shule mbalimbali zilizopo katika halmashauri za mkoa wa Tanga ambao walipata mafunzo waliishukuru serikali kupitia BAKITA pamoja na shirika la urithi wa utamaduni wa kiswahili (SUUKI) kwa kuwajengea uwezo na maarifa ya jinsi ya kufundisha lugha ya kiswahili kwa wageni huku wakiahidi kwenda kuwa mabalozi kwa wengine.
"Tunalishukuru shirika la SUUKI Pamoja na serikali kupitia BAKITA , baada ya kupata mafunzo haya yametufaidisha sana tutakwenda kuyafikisha vyema kwa walengwa vyema kwa wageni na wenzetu pia tuiombe serikali iweze kuweka sera rafiki ili tuweze kukuza lugha yetu" walisema washiriki hao.
Jumla ya walimu 12 wa somo la kiswahili kutoka halmashauri za mbalimbali za mkoa wa wamepata mafunzo yaliyodumu kwa wiki moja ya kuwajengea uwezo wa kufundisha lugha ya kiswahili kwa wageni ambapo pia waliweza kupewa vyeti wakitumwa kwenda kuvitumia vyema elimu hiyo.



0 Comments