Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Tanga,Rajab Abrahaman Abdalah akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao cha Halmashauri Kuu ya mkoa.Mkuu wa mkoa wa Tanga Waziri Kindamba akizungumza kwenye kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Mkoa.
Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Tanga Suleiman Mzee akizungumza kwenye kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Mkoa.
*********
Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tanga iliyokutana 04/07/2023 katika kikao chake cha kawaida chini ya Mwenyekiti Rajab Abrahaman Abdalah imeazimi kutoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa alizofanya kwa Watanzania kwa Mkoa wa Tanga.
Kazi kubwa zilizofanyika katika mkoa wa Tanga ni kama ifuatavyo
1.Upanuzi mkubwa wa Gati la Bandari ya Tanga ili kukuza uchumi wa Wanatanga na Watanzania wote.
2.Kuongeza Bajeti ya kugaramia Elimu bila malipo kwa Watanzania wanyonge na wenye kuhitaji elimu kwa maendeleo na manufaa ya kila mmoja.
3.Kulipia na kuleta ndege ya Mizigo ambayo kwa Tanzania ni mara ya kwanza kuwa na ndege maalum ya Mizigo.
4.Kuendelea kuimarisha na kudumisha mahusiano baina ya Tanzania na Nchi za wenzetu na mataifa makubwa yaliyoendelea.
5.Kusimamia na kuimarisha hali ya Ulinzi na Usalama katika nchi yetu,wananchi wafanye kazi kwa usalama na kujiongezea kipato kwa maisha yetu.
6.Kuongeza na kuleta fedha za maendeleo kwa mkoa wa Tanga kiasi cha shilingi 356,830,194,471.45
7.Kutuletea chakula cha bei nafuu kiasi cha Tani 2,675 ambazo zimegawanywa katika wilaya za Mkinga,Handeni,Korogwe,Kilindi na Lushoto kwa bei ya shilingi 970 kwa kilo.
8.Chama cha Mapinduzi(CCM)mkoa wa Tanga inampongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kitendo cha kiungwana cha kuondoa Tozo ya miamala katika mitandao ya simu.
Mbunge wa viti maalum mkoa wa Tanga Husna Sekiboko akiwa kwenye kikao hicho cha Halmashauri Kuu ya Mkoa.
0 Comments