ULAYA HALI TETE UFARANSA YAKATIWA GESI

Vita vya Russia na Ukraine vikiendelea na vikwazo vya nchi za Magharibi vikiwekwa Moscow,mauzo ya gesi ya Russia kwa Ulaya yamepungua sana na kuziacha nchi nyingi za bara hilo zikikumbwa na tatizo la kujidhamini nishati na kuongezeka gharama ya bidhaa hiyo,Shirika la gesi la Gazprom la Russia limetangaza kupunguza kwa asilimia 50 mauzo ya gesi kwenda Italia. 

Mtiririko wa gesi katika mitandao ya usambazaji wa nishati kwa nchi zingine za Ulaya pia umekatishwa vyanzo vya Ufaransa vimethibitisha kwamba nchi hiyo haijapokea gesi kutoka Russia kupitia bomba.

Kampuni ya Usafirishaji wa gesi ya Ufaransa GRTgaz imesema kuwa mtiririko wa gesi ya Russia kupitia Ujerumani umesitishwa na kwamba nchi hiyo haijapokea gesi yoyote kutoka Russia kupitia bomba hilo tangu Juni 15,Ufaransa ambayo inategemea sana nishati ya Russia  inadhamini takriban asilimia 17 ya gesi inayotumia kupitia mtandao uliounganishwa na Ujerumani.

Wiki iliyopita Gazprom ilionya kwamba itapunguza kwa kiasi kikubwa usambazaji wa gesi kwa Ulaya kutokana na masuala ya kiufundi yanayotokana na vikwazo vya Magharibi,Gazprom inahusisha masuala hayo na ucheleweshaji unaofanywa kwa makusudi na shirika la Ujerumani la Siemens,ambalo limejiunga na vikwazo vya Magharibi dhidi ya Russia. 

Usambazaji wa gesi ya Russia kwenda Ulaya kupitia bomba hilo umepungua kwa asilimia 60 wiki hii,na hivyo kusababisha bei ya gesi barani Ulaya kupanda sana.

Katika kipindi cha miezi michache iliyopita,na kufuatia kuanza vita vya Russia na Ukraine nchi za Ulaya zimebuni na kutekeleza vifurushi mbalimbali vya vikwazo kwa ajili ya kutoa mashinikizo dhidi ya Russia.

Lakini vikwazo hivyo sasa vimefanya mambo kuwa magumu kwa nchi za Ulaya zenyewe,ambazo zinategemea sana rasilimali za nishati za Russia.

Pia bei ya mafuta barani Ulaya imepanda kwa kasi kubwa na hivyo kusababisha bei za bidhaa na huduma nyingi kupanda,huku nchi nyingi za bara hilo zikikabiliwa na mfumuko wa bei na kushuka kwa ukuaji wa uchumi. 

Bei ya saa moja ya megawati ya gesi asilia katika masoko ya Ulaya, imefikia euro 130,hii ni katika hali ambayo bei hiyo wiki iliyopita ilikuwa euro 100 na mwaka uliopita euro 30.

Post a Comment

0 Comments